Uzima Liwaza
Homepage

 kifaransa   kiitaliano   kijerumani   kihispania   kiingerrezza   Russan language  
Uzima Liwaza, Würzburg, Germany


LammManeno ya Baba

yakushauri

wewe nawe

 • Je, unawezaje kupata uzuri, usafi, upendo na mlingano wa ndani?
 • Kifo
 • Kujifanua mwenyewe hukuletea uhuru
 • Kutoa pasipo kujipendelea
 • Mawazo ya kujipendelea
 • Na uikomboe nafsi yako mwenyewe
 • Kaa ndani Yangu, ndani ya Mwanga Wangu
 • Mawazo yako na yalingane na maneno yako
 • Na uishi ukizingatia
 • Uwe Bibi Arusi Wangu
 • Kweli wewe ndiwe mpenzi Wangu
 • Mimi Ndimi
 • Na uikomboe nafsi yako
 • Milele, Roho ndani ya vyote, hukuhudumia wewe
 • Kutoa huleta uhuru
 • Sadaka
 • Na uyasafishe yote yanayokubughudhi
 • Ushike njia pamoja Nami, Mimi Ndimi Msindikizi wako
 • Mimi Ndimi Upendo
 • Na uuone Uhai katika vyote
 • Unavyofikiri, ndivyo wewe ulivyo
 • Baba na Mimi ti Umoja
 • Uzima Liwaza

UZIMA LIWAZA

Tunaishi katika kipindi cha mabadiliko makubwa kabisa. Watu wengi walio tayari rohoni wanahisi ya kwamba hiki ni kipindi muhimu katika historia ya mwanadamu kilichoanza hivi karibuni.

Kuzikiuka Sheria Takatifu, Amri kumi za Mungu na Hotuba ya Mlimani, kwa muda wa miaka elfu nyingi, kutakuwa na madhara yake. Vita, maafa ya maumbo asilia na vurumai vimetabiliwa.

Kristo anapenda kutulinda kutokana na mabaya. Kristo hawaachi wafuasi Wake.

Katika Uzima Liwaza, Kristo amejenga msingi ambao, Yeye, Mwana wa Aliye Juu, anakusudia kuwaongoza watu wote. Yeye anatupatia sisi Mkono Wake, Maongozi Yake Mwenyewe!

Katika Uzima Liwaza, anayatimiza yale aliyowaambia wafuasi Wake, miaka 2000 iliyopita: "Hata bado Ningali Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini Yeye atakapokuja, Huyo Roho wa Kweli, atawaongoza awatie kwenye Kweli yote." (Yohana 16,12)

Hivi leo, Kristo hatupatii maelezo ya matayarisho tu kwa Wakati Mpya, yaani Wakati wa Kiroho, uliobashiriwa na manabii wengi katika miaka elfu nyingi iliyopita, bali anakusudia pia kutuongoza kwa dhati katika Wakati Mpya kupitia nabii Yake wa kike.

Anakusudia kutuongoza dhidi ya giza la kiroho, dhidi ya nafsi yetu inayojipendelea, kuelekea katika uhuru wa ufunuzi wa kina cha roho, ambao tutaufikia kupitia kuzitekeleza na kuzitimiza Amri Takatifu. Uhuru huu hutuletea Upendo usiojinafsisha, Ukweli, Hekima na Nguvu inayoyaangaza matendo mlingano ya kikristo.

Namna mpya ya wanadamu itachipuka kutoka katika kuzitekeleza Sheria za Kiroho. Namna hii ya watu, ambayo inapenda Amani na Huruma na yenye Ujazo wa nguvu itakuwepo katika Ufalme wa Mungu Duniani, yaani Dola ya Kristo itakayoonekana popote Duniani baada ya badiliko la kipindi.

Hata hivi sasa, msingi wa Dola ya Kristo unajengwa kulingana na maelekezo ya kiroho. Ufalme wa Amani unajengwa kupitia watu walioufungua mlango wa Ufalme wa Mungu ndani yao.

Watu hawa wanaifuata kwa dhati Njia ya Ndani, ambayo hivi sasa inafundishwa na Kristo na Mtumishi Wake, Kerubi wa Hekima Takatifu katika Uzima Liwaza.

Mawingu haya meusi yanayotanda kwenye upeo wa macho wa wakati huu ndio mavuno ya mbegu iliyopandwa na ubinadamu.

Mwana wa Mungu atatuongoza kando kando ya Mavuno haya hadi tumefika salama. Yeye Ndiye Njia! Yeyote ana-yemkubali Kwake Yeye, huyo hakuna mapinduko, bali atapenya katika Wakati Mpya.

Kwa ajili hii, Bwana anakusudia kuwaandaa walio Wake, kila mtu! Roho Mtakatifu katika Kristo, na Mtumishi Wake, Kerubi wa Hekima Takatifu, wana-tupatia ufunuo juu ya kanuni za kuumbwa dunia. Tunafunukiwa na Kristo, Naye anatuonya, ili tuzitimize Sheria Takatifu, kwa ajili hii, Baba, Muumba wa nafsi zote zilizo hai, alitupatia, na hata sasa anatupatia Mashauri Yake ya Asili yenye Nguvu na Ujazo.

Wakati ujao tayari umekwisha anza katika Uzima Liwaza. Kujimudu kikristo kwa Wakati Mpya kunastawi kutokana na hayo yote:

Uhuru, Umoja, Udugu.

Marafiki wa Kristo katika Uzima Liwaza
Würzburg, Februari 1986


[ Book Index ] [ Universelles Leben ] [ Mail ]
[ Order Free Info ]


Universelles Leben e.V., P.O.Box 5643, D-97006 Würzburg
Germany Phone: (+49) 931-3903-0 , Fax: (+49) 931-3903-233
email: info@universelles-leben.org
12708