Uzima Liwaza
Maneno ya Baba


Maneno ya Baba
yakushauri
wewe nawe

Kristo, Ndiye Aliye
Ufunguo wa Lango la Uzima
Uzima Liwaza

First Edition 1993

Publisher:

© Universelles Leben

Haugerring 7
97070 Würzburg
West Germany

script no. s108su

original title:
Vaterworte auch an Dich

The German edition is the work of reference for all
questions regarding the meaning of the contents.

All rights reserved.

Yamefunuliwa na
Roho Mtakatifu wa Mungu
kupitia kwa Nabii wa kike
wa Bwana

Gabriele, Würzburg

DIBAJI

Maongozi

Maongozi yatokayo katika Uzima wa milele, kutoka katika chemchem ya Ukweli, Ujazo wa Mbingu zote, kutoka katika Ufahamu wa juu kabisa wa Mbingu.

Kwa kutumia kijitabu hiki tunabahatika kusikia maneno Yake Mwenyewe Baba, kwa mwanawe. Maneno haya pia yanaelekezwa kwetu, tuyakubali na kuyapokea.

Kwani Mungu, Roho Mtakatifu, Baba yetu sote, anayetuwezesha hata tukaachana na kujipendelea sisi wenyewe, Yeye atupendaye daima, na Aliye nasi kwa kila mmoja wetu, anatushauri kila wakati, katika kina cha nafsi ya roho ya kila mmoja wetu. Tukikubali kuenenda katika Njia ya Ndani ya kiroho, na kama tukihitimu kupata vidato kadhaa vya ustawi wa juu ya kiroho, basi nasi tutapata ufunuo huu wa kiroho katika nafsi yetu wenyewe.

Kutokana na ustawi huo, ndipo mtiririko wa Utukufu utakapopenyeza katika chembechembe hai za ubongo, kwa njia ya kimoyo rohoni mwetu na katika sehemu zilizokamilika uchujo wa kiroho. Chembechembe hai za ubongo zitakaposafishwa kutokana na fikira na mawazo yote ya kibinadamu, tayari zinaweza kumtumikia Yeye Bwana. Roho Mtakatifu wa Mungu, Ufahamu Mtimilifu vitawasiliana nasi pamoja katika utakato na usafi wa "Mimi Ndimi". Ufunuo huu wa Roho Mtakatifu wa Mungu utokao kwa Njia ya kiroho, ambao kila mmoja wetu huweza kuupata, umekusudiwa kwake mwana mwenyewe tu, kwa maana huo sio Ufunuo wa Mjumbe Mtakatifu.

Yaani Ufunuo huu wa Mjumbe Mtakatifu wa Mungu ni sauti ya Roho Mtakatifu wa Mungu itokayo katika Njia ya roho na ya mwanadamu. Mashauri haya Yake Baba, yenye kupenyeza vema kwenye roho na mwili, hayakusudiwi kwa mjumbe tu, bali kwa watu wote walio tayari kuyapokea.

Nabii wa kike wa Bwana anatuwezesha kunufaika na zawadi zitokazo kwa Roho Mtakatifu wa Mungu, ambazo amebarikiwa kuzipokea.

Nasi na tuukubalie Ufunuo huo, tukishukuru kwa yote Mwenyezi aliyodhamiria kutuonyesha.

Mkristo katika Njia ielekayo kwa Mola
katika Uzima Liwaza

Mimi Nipo nawe

Njoo Kwangu wakati wowote.

Ungamana kwa chochote kile na Baba yako, Ambaye Roho Wake Mtakatifu Yupo nawe. Mimi Niliye Uhai, ninakusudia kukuongoza na kukulinda.

Popote ulipo, Nipo Nami pia, kwani Mimi Nimo ndani yako na katika nafsi zote za Uhai.

Moyo wako na uangaze upendo kila wakati, ndipo utakapoungamanishwa Nami, kwani Mimi Nimo katika namna zote za Uhai, Ndimi Roho Mtakatifu wa Baba yako.

Na usiogope

Mimi, Baba yako, Ndimi Upendo.

Umeumbwa kutokana na Ufahamu Wangu wa milele. Ufahamu wa Uhai wa milele ndio maisha yako pia.

Tazama, roho yako hafi, bali vinavyotakiwa kufa ni ubinafsi wako, hamu zako na makusudio mabaya. Jinsi yanavyopungua ndivyo Mimi nitakavyoutakasa mwandani wako.

Kwa hivyo, pindi utakapojitambua ya kwamba umepata huo utakaso, ndipo unapokuwa na maisha ya kweli.

Nitamtakasa yeyote yule atakayenitakasa; naye atajitambua kuwa yupo Nami, Nami Nipo naye. Mwanangu, hayo ndiyo maisha ya kweli, yaliyo mbali na hofu ya kutisha, dhambi na kifo.

Na usitende dhambi

Mwanangu, matendo ya dhambi ni kwenda kinyume cha Sheria ya Mungu, Baba yako.

Tendo lolote lile lisilolingana na Sheria Yangu Takatifu, ni dhambi. Wote wanipendao Mimi ni wale wanaokubali Mashauri Yangu wanaozitimiza Sheria za Uhai.

Ukinipenda kweli, ndipo utakaposhuhudia ya kwamba hisia zako, mawazo na maneno yako vinasafishika, tena matendo yako yawe mema na maisha yako yasiwe ya kujipendelea.

Ndipo nafsi yako itakapojazwa na mwanga wa ukweli. Na uzuri wa mwandani wenyewe utakapojionyesha katika umbo la nje. Utafaidika kupata uchangamfu na ufichuo wa kiroho.

Ndipo utakapokuwa ndiwe nafsi uliyejazwa na Bubujiko Langu na Mwanga Wangu angavu, mwanga ambao huangaza kwako na mionzi yake hupenyeza hata kwa jirani yako.

Mwanangu, hayo ndiyo Mapendo yaliyo safi, yanayokupatia uhuru. Matendo ya dhambi huifuga na kuifunga roho katika jela ya mawazo na matakwa ya kibinadamu.

Upendo Mtimilifu huleta uhuru na uzuri. Humkamilisha mwanadamu kwa upevu wa roho iliyo safi.

Na ujitakase na utakuwa na uhuru

Mwanangu, usafi wa roho humletea mwanadamu utiifu na ubora.

Yeyote yule apendaye hutoa; na huyo atoaye hujinyakulia uhuru. Tazama, mwenye kutoa ndiye mwenye uhuru na ukweli, ameachana na chochote kinachopendwa na chenye thamani kwa mchukuaji. Mtoaji huangalia tu sura ya mchukuaji na kutambua mahitaji yake. Kwa hivyo, utoe kwa wale walio na dhiki, na hapo vilevile utakuwa umenipa Nami, Mtoaji wa milele.

Yule atoaye yu karibu na Mtoaji, yaani Upendo, unaoifungua roho kutokana na minyororo ya tamaa, wivu na uchoyo.

Mwanangu, ni mtoaji tu, mwenye uhuru wa kweli. Utoe na utapokea upendo na uhuru kutoka Kwangu. Katika kutoa bila ya kujipendelea, yule mhitaji asiyejipendelea hupata haki za Mungu Mwenye kujua kumlinda na kumhifadhi mwana Wake.

Uangalie mashomoro, hawakusanyiki na kuvuna, wala hawahitaji kuweka nafaka katika maghala, hata hivyo hao hutunzwa, na wanao uhuru kutoka kwa Mwenyezi Mpaji.

Na uangalie maua ya mashamba, yanamea pasipo kuuliza, kwa nini inanyesha na hayo maji yanayoyastawisha yanatoka wapi.

Lo tazama, wao wanamhisi Mwenye haki zote, Mwenyezi Mwenye kutoa Uhai, Ndiye Mimi Ndimi katika Uhai wote.

Na uwe mkweli katika nafsi yako

Mimi Ndimi Upendo, Ndimi Roho Mwenye Haki zote. Na uwe mkweli katika nafsi yako, ndipo utakapoipata njia ya kufika Kwangu, Niliye Upendo.

Tazama, ninakuongoza katika maono na mawazo yasiyofaa, katika maneno yako ambayo mara nyingi hayalingani na maono wala wawazo yako. Mara ngapi mtu hunena kinyume anavyowaza. Kufanya hivyo ni unafiki na wala siyo uaminifu. Mwanangu, tazama, katika kufanya hivyo ndivyo chanzo cha kumzuia mwanadamu kuwa mwenye uhuru na mwenye upendo kamilifu. Mwenye unafiki si mjanja, hukusudia kuficha kile ambacho kinajulikana machoni Mwangu. Ingawa amejionyesha kuwa mjanja kwa muda fulani mbele ya jirani yake, Yeye ajuaye mambo yote atayafunulisha yote kadri ya kanuni ya kupanda na kuvuna.

Uwe mkweli katika nafsi yako. Nena lile linalolingana na jinsi tu unavyohisi na kuwaza.

Iwapo utamudu kufanya hivyo, basi Mwanangu, ndipo mara kwa mara utakapojikagua kila siku, na hivyo kutua mizigo yote kwenye Mwanga uponyeshao wa Baba yako; hata mwenendo wako uwe bora pia na hisia na mawazo yako yawe yenye utiifu.

Mwenendo wako ukiwa bora, ndipo utakaponena lililo jema na bora tu. Maadam mwenendo wako unapevusha hisia na mawazo yako, kwa hivyo hisia na mawazo vinalingana na maneno yako.

Tazama, huku ndiko kufanya haki kwako wewe.

Mwenendo mtiifu huongoza katika kazi na uchumi bora

Afikiriaye juu ya wema na ubora, atajihusisha pia katika shughuli halali. Tazama, Mwanangu, wakati huu duniani kuna biashara walakini katika Uhai wa milele, hakuna.

Binadamu huhitaji mengi ambayo tayari roho imekwisha kuwa nayo hapo awali, kama zawadi kutoka kwa Mtoaji wa Uhai wa milele.

Binadamu huhitaji chakula na mavazi, malazi na vitu vingi vinginevyo. Roho iliyo na utajiri wa mbingu ndani yake, haina budi mara nyingi kulazimishwa kusumbuka kwa ajili ya kokwa, mwili yaani mwanadamu, anavyohitaji, anavyoazimia na kukusudia.

Matendo ya kibiashara pasipo kujipendelea huleta vilevile mwenendo mwema maishani. Yeyote yule afanyaye shughuli za kibiashara katika maana ya kutojipendelea mwenyewe, huyo ataenenda na kuingia ndani Yangu, Ndimi Mwenye Haki zote.

Lo tazama, mtu mwenye utambuzi mwema ni yule aliye safi na bora na anayefanana Nami, Mwenyezi. Mwenendo mwema aishio nao mwanadamu duniani humletea uhuru yeye na roho yake.

Uhuru

Mwanangu, kuwa na uhuru kuna maana ya kuondokana na ubinadamu.

Kuwa na uhuru kuna maana gani? Pindi juhudi za mwanadamu ni kumpendeza Mungu tu, kwa hivyo hataiga maoni ya jirani zake. Tena hatapendelea wala kuyaiga matashi na tamaa za jirani zake. Maadam mapenzi yake ni kumpendeza Mungu, kwa hivyo atanijia hatua kwa hatua karibu Nami, yaani Mwenye Milele.

Lo tazama, katika matendo ya kujitosheleza binadamu mwenyewe, yamo kujiona na kujitia makuu. Huku ndiko kunakosababisha utoshelezi wa kibinadamu. Lakini katika kujitosheleza huku, hatimaye uhai wa kiroho husimamishwa, na kwa hivyo kuifanyia roho kufungwa na kupunguzwa.

Yeyote apendaye kuwa na uhuru hana budi kuniangalia Mimi tu na kufuata kwa bidii lengo la roho yake. Asiwe vuguvugu, kwani kuwa vuguvugu kunasababisha kuanguka mbali Nami, na hivyo hufungua lango la mafikara binafsi.

Kuwa na uhuru kuna maana ya kuungana Nami katika maneno na matendo. Hizi kweli ndizo mbegu zizaazo mavuno mema kwa wote, yaani yule mfuasi wa Mungu na jirani yake, mwana Wangu.

Mbegu iliyo bora

Mwanangu, maisha ya kweli ndiyo kutoa.

Kwa hivyo kutoa ni vema zaidi ya kuchukua. Kutoa huleta uhuru kwa roho na kwa binadamu.

Katika tendo la kutoa kupo kujitoa, kujitolea, yaani toleo thahibu katika vyote vinavyopendezeshwa na kukusudiwa na mwanadamu.

Tazama, tuzo lisilo na choyo katika maneno na matendo ndilo mbegu iliyo bora ambayo huzaa matunda yake. Matunda hayo mema hayatarejeshwa tena ardhini, kwani tunda lililo bivu, daima huchukuliwa na mhitaji. Uhitaji huu ndio Roho wa Uhai wote, avunaye tunda hilo na kulihifadhi katika ghala timilifu, pahali pa milele, ambapo ipo hifadhi ya Uhai timilifu.

Na uwe kama tunda lililoiva

Yule atakaye kuiva kwenye mti wa ufafanuzi hana budi kujitolea, siyo tu kwa ajili yake mwenyewe, bali kwa manufaa ya wote. Kwani kila mmojawapo hana budi aubebe mzigo wa mwenziye.

Mwanangu, katika kujifafanua mwenyewe, roho hukomaa.

Ufafanuzi na kujitolea kwako mwenyewe hakutoshi kukuwezesha wewe kuingia katika nyumba ya Baba. Ila kutokana na tendo la upendo la kujitolea kwa jirani, yaani tendo la upendo la hiari lisilo la kujipendelea, tendo la utumishi, huifungulia roho lango la Ufahamu wa Milele, karibu Nami, Kwake Yeye, Niliye Ndimi, yaani Uhai.

Tendo la upendo la kujitolea kwa jirani

Tendo la kujitolea bila ya kujinafsisha ndilo maisha halali. Tendo hilo huifungulia roho minyororo ya nafsi yako. Kwa hivyo wewe na roho yako utapata kuungana na mioyo ya wale wanaonitafuta Mimi kwa dhati.

Tendo la upendo la kujitolea lina maana ya kujitoa mwenyewe, kutokujifikiria mwenyewe, kutokuweka madai wala matashi, bali kujikabidhisha kwa Mungu na kwa jirani yako. Hiyo ndiyo sadaka ya dhati, huo ndio Ushujaa wa Ufahamu.

Yule ajitoleaye pasipo kujinafsisha hunufaika zaidi kuliko anavyofikiria. Nami nitakuwa naye kumpa mahitaji yake na yote muhimu anayoyahitaji kwa yeye na kwa wokovu wa roho yake.

Ushujaa wa dhati

Mwanangu, ushujaa unaonyeshwa na yule tu mwenye kujisahau mwenyewe. Na ni yule ambaye alishakwisha kuisahau nafsi yake, ndiye mshujaa.

Ni ndogo na ni pungufu iliyoje nafsi ya mwanadamu, binadamu ambaye fikra zake na matendo yanamzunguka yeye mwenyewe, ambaye hujihusisha tu na manufaa yake mwenyewe.

Lo tazama, kwa kila ulifikirialo na ulitendalo leo litakuwa mbegu kwa kesho.

Kwa hiyo, mtu tajiri mwenye kujali mambo yake na manufaa yake mwenyewe tu, kulingana na mwenendo wake, basi atajavipoteza vitu vyote punje hadi punje, hata hatimaye kubakia maskini wa mwili na roho kiasi kwamba atajalazimika kuishi kwa kuombaomba, aidha itamlazimu kufanya kazi ngumu mno kwa mahitaji yake hayo.

Mwanangu, kila mmoja hupokea kulingana na jinsi anavyofikiria na anavyoenenda.

Na upokee Ukamilifu

Yeyote yule mwenye kukusudia kuupokea Ukamilifu, Mimi, Mwenye Nguvu zote na Ujazo, hana budi kuipoteza nafsi yake mwenyewe, hana budi kujitolea kama zawadi.

Lo tazama, mtajiri ni yule tu anayejitolea nafsi yake kama sadaka kwa manufaa ya binadamu. Mwanangu, huyo hataishi pahali duni wala hatalazimika kuishi pale, kwa sababu amekwisha upokea Ujazo kutoka Kwangu, na amefanikisha kile anachowajibika kama mwana wa Baba yake.

Huyo atakipokea kila kitu anachokihitaji na zaidi, kutokana na kanuni za maumbo asilia za dunia hii.

Utajiri wa dhati

Utajiri wa dhati ndio nuru ya roho yako inayopata hisia za Roho Mtakatifu wa milele ndani yake, roho ambayo ipo pamoja Nami, Roho Mtangulizi. Mwana huyo hatapungukiwa, atapokea kutoka Mikononi Mwangu na atashiriki katika sherehe kubwa ya Uhai, siyo tu huko mbinguni bali tayari hapa duniani.

Mwanangu, una shida gani? Hunao utajiri wa nje - kama walivyo matajiri wa ulimwengu huu. Unaumiliki utajiri wa ndani. Kila unachokihitaji katika maisha haya ya nje, tayari nimekupatia, na hata zaidi.

Lo tazama, wana katika ufalme wa Uzima wa kiroho huishi katika ujazo. Watu hupata kile wanachohitaji na hata zaidi, yote kulingana na nuru ya roho zao. Mwanadamu hawezi kuupokea ujazo kamilifu wa makao ya milele kama zawadi, maadam dunia imesongamanishwa na kwa hivyo imejiwekea mipaka yake katika muda na nafasi. Wanadamu wengi huishi katika nafasi hii na muda huu na kwa hivyo sayari ya dunia imejazwa mno na idadi kubwa ya watu. Hata hivyo yeyote yule auamshaye uangafu wa ndani kupitia Uzima ndani Yangu, huyo pia atakuwa na utoshelezi duniani na wala hatapungukiwa kitu.

Mimi, Niliye Mtoaji

Mwanangu, na ustawi katika sura ya Ufahamu Wangu!

Lo tazama, Upendo Wangu hutiririka bila kikomo! Ninatoa bila kuchoka nguvu za Upendo kwa Uzima wote. Kulingana na ufahamu wa ustadi wa kila roho, roho hizi hupokea Nguvu Yangu. Kila mmoja hurusiwa kupokea kutoka kwenye Utiririko wa Upendo, walakini kila mmojawapo anaweza kuchukua kiasi tu kile kilinganacho na kiwango cha ufahamu wake.

Ufahamu wa ustadi wa roho unaweza kufananishwa na ua linalojikunjua. Jinsi ua linavyojikunjua na kujifunua zaidi kuelekea kwenye mwanga wa jua, hivyo pia mionzi mingi ya jua itaingia ndani yake ua. Lo tazama, Mwanangu, jinsi mwanadamu anavyojifunua mwenyewe zaidi kwa ajili ya Upendo Wangu, hii ina maana kwamba, ndivyo zaidi anavyojimudu kutokujipendelea, basi vilevile yeye hupokea nguvu zaidi kutokana na Wokovu Wangu na Nguvu Zangu ziletazo Uzima.

Upendo hutolewa daima kwa usawa. Upendo hutiririka kwa kila nafsi za Uhai: kwenye roho za vizuka, kwa wanadamu, kwenye roho, kwa wanyama, mimea na mawe. Nafsi zote hizi hupokea Upendo.

Jinsi nafsi yako inavyozidi kujimudu kutokujipendelea na hivyo kuangaza zaidi, ndivyo hivyo inavyoweza kupokea na kutoa kwenye chemchem ya kisima Changu.

Mwanangu, na uyashuhudie haya: Kutoa ndiko bora zaidi kuliko kuchukua! Yule atoaye pasipo kujipendelea hupokea yote kwa umaridadi kutoka kwenye chemchem ya Upendo wa Milele.

Mimi Ndimi Upendo

Mimi Ndimi Upendo mkamilifu.

Ninakuona tu wewe kama mwana mkamilifu wa Upendo Wangu. Dosari zitayeyushwana kuondoshwa kutokana na nguvu ya kanuni ya vyanzo na madhara, walakini sio kwa Upendo mkamilifu.

Mwanangu, na ustawi katika taswira Yangu! Na uwaangalie tu wenzako kutoka katika kilele cha ufahamu wa Upendo mkamilifu! Na uwaangalie wao kama nafsi kamilifu! Na usiyaangalie makosa na mapungufu yao! Na usamehe!

Yule mwenye kudiriki katika yote kwa Ukamilifu, uzuri na ubora kwa dhati, huyo huyaona yote kwa macho ya upendo. Na yule mwenye kudiriki katika kilele cha upendo, huyo kwa hakika atakuwa mpevu na mwenye kujaa upendo.

Ndipo uzuri, wema na upendo mkunjufu hupenyeza ndani ya mtu huyo. Huyo ndiye ambaye angeweza kuubadilisha ulimwengu kwa ubora zaidi kadri vya kutosha, ikiwa ulimwengu ungemsikiliza huyo na ungejikagua na hatimaye kuishi kutokana na ushuhuda wake huyo.

Na ustawi katika chapa Yangu

Mwanangu, maisha ni mazuri ndani Yangu na pamoja Nami!

Na uwe mwenye ucheshi mzuri: matumaini, upendo na uvumilivu! Lo tazama, malaika wa mbingu wapo pamoja nawe na pamoja na wana Wangu wote wanaoiinua mioyo yao Kwangu na ambao kila siku roho zao zaidi na zaidi huzitakasa kutokana na machafu yote, na uduni wa ulimwengu huu.

Yule mwenye jitihada kuelekea kwa Aliye Juu kabisa, huyo pia hupokea kutoka kwa Aliye Juu kabisa.

Mwanangu, na uwe mpevu na mwema! Daima ujiangalie ndani yako na uniulize Mimi, Bwana na Mungu, ndani ya vyote. Lo tazama, kulingana na ufahamu wako ninakusudia kukujibu, kwani Mimi Ndimi Vyote katika vyote. Na uyatambue haya!

Mwanangu na uyafuate mashauri Yangu, ndipo utastawi na kumea kila siku zaidi na zaidi!

Lo tazama, Upendo Wangu, Neema Yangu kamwe hazikuachi. Mimi, Bwana wako hukuongoza hadi kwenye kilele cha amani, pahali ambapo Jua la milele hukupatia tu wewe, wokovu na upendo.

Kila chembe ya roho huhitaji Mwanga Wangu mtimilifu. Mara tu chembe nyingi za roho na chembechembe hai za mwili wako zinapokuwa angavu, ndipo hivyo ndani yako kumekwisha kufanikishwa.

Kwa hivyo vilevile, wewe ndiwe chembe hai ya Mwili Wangu. Lo tazama, chembe hiyo ni angavu na nyeupe: mfano wa rangi nyekundu mara jua linapochomoza, nafsi yako hunawirika katika upeo wa macho wa Uhai Wangu. Nia zako zimo ndani Yangu, Nami hizo ninazitumia, kwa hivyo Nimo ndani yako na ufahamu kuwa, Mimi Ndimi Vyote katika vyote. Tazama, maarifa haya na yakupatie nguvu na liwazo katika siku za kujitolea mwenyewe.

Jua la Haki ndilo burudani ya roho yako. Hivyo unaruhusiwa kuungana katika tenzi na nyimbo za roho yako, zinazosema: Mimi nimo ndani yake Mungu, Aliye Baba yangu, na Baba yangu Yumo ndani yangu kwa dhati. Nimeugundua undani wangu na ninahisi ukamilifu wa roho yangu, yaani mwili wa kiroho unaolingana tena na chapa ya Baba yangu. Shukrani na ziwe Kwako, Lo Bwana, na Mwana Wako.

Na ushukuru katika furaha na huzuni

Mwanangu, na ujifunze kushukuru ipasavyo!

Lo tazama, katika shukrani za dhati kuna furaha isiyoisha na udugu usiojinafsisha. Katika shukrani za dhati zinazotoka katika kina cha roho yako, na zinazopaa Kwangu, Mwenye Milele, kuna ushujaa wa kweli. Yule mwenye kushukuru katika vyote, hata katika ugonjwa na dhiki, huyo huiamsha roho yake ndani Yangu, Roho Mtakatifu wa Uzima.

Shukrani kunjufu na za dhati hutoa burudiko la roho na mwili. Mtu atoaye shukrani huisahau nafsi yake mwenyewe. Mwanangu, tendo hilo la kuisahau nafsi yako linaiamsha nguvu Yangu ndani yako. Nguvu yenye kukuwekea kila kitu kwa utaratibu na kukutakasa, nguvu inayoyayeyusha na kuyaondosha mengi.

Lo tazama, Mimi Ndimi Huruma pia. Na ustawi katika Huruma, nawe utakuwa mtumishi mwema wa binadamu.

Utumishi mwema

Katika tendo la kuisahau nafsi yako kuna ushujaa wa kweli, utumishi mwema.

Yule aliye mtumishi mwema wa binadamu hajitumikishi kwa ajili ya pesa na mali yenyewe. Ni mwenye kujitolea kwa ajili ya jirani yake.

Lo tazama, huu pia ni ujasiri wa kweli, ndio ushujaa wa dhati.

Ujasiri wa dhati

Mjasiri wa dhati ni yule atoaye kila kitu, naam, hata Uhai wake kwa ajili ya kondoo wake. Kwa hivyo, Mwanangu, ndivyo nilivyokuwa nimeishi, nimependa na nilivyotoa, Ndimi Bwana na Mwokozi wako.

Sasa na uwe hodari, na unifuate Mimi! Jipe moyo kuubeba msalaba wako na utambue kwamba nitaubeba mzigo wako pamoja nawe iwapo unaniamini na kujikabidhisha Kwangu, ikiwa ni pamoja na dosari na unyonge wako, na uviachie hivyo vyote Kwangu Mimi, Roho wa Kristo. Njoo, unifuate Mimi!

Na unifuate Mimi

Yule anifuataye Mimi, ataweza kuvumilia vingi, hata masuto na lawama za wenzake. Yule mwenye kunifuata Mimi kwa dhati hataongelea juu ya dosari na unyonge wa wenzake. Na wala hatazishikilia hamu zake potofu kwa kuzifikiria na kuzihofia.

Yule anayeutimiza ufuasi wangu, daima hutoa, hata kama ni kutoa pasipo kikomo. Yeye ndiye mwanga ndani Yangu, Nami ninaangaza kupitia kwake. Kwa hivyo huyo anao uwezo wa kuyavumilia mengi, na kwa wengi.

Mimi Ndimi Mchungaji Mwema. Wewe uwe kondoo Wangu, na usiwe tu kondoo Wangu, bali pia uwe kama mwanakondoo!

Na uwe mwenye uwezo wa kuvumilia

Huzuni unazozikabili kuzivumilia hivi sasa ndizo dosari zako zilizoilemea roho yako wakati wa maisha haya au katika kipindi chako cha maisha yaliyopita. Hivi sasa unayo ruhusa ya kuondokewa na dosari zako.

Na uzikubali huzuni na ushukuru, kwani katika kukubali na kushukuru huku, wewe unapokea nguvu ya kuzivumilia huzuni hizo nisizoweza kuziondosha kutoka kwako, kwa sababu huzuni hizo ni kwa ajili ya wokovu wa roho yako. Mwanangu, huzuni zinazobaki ambazo huna budi kuzivumilia, hizo zinakupatia wewe ufafanuzi mpya katika njia yako.

Na uvumilie, ujifafanue na ukomae, na kwa hivyo utamea katika kuelekea Kwangu na utasafishika kuufikia ukamilisho. Tazama, ninachuma tu matunda yaliyoiva; matunda yaliyo mabivu kabisa na kuyabeba kuyarejesha katika Utukufu wa Mungu, katika amani ambayo ulimwengu hauijui.

Ulimwengu haunijui Mimi

Ulimwengu sio dunia. Ulimwengu ni ule wote ambao huishi kwenye dunia na usiojinyanyua kwa Mungu, Mwenye Enzi. Ulimwengu huu unao walimwengu wanaofikiri kuwa sayari ya dunia ndiyo tu iliyo kweli na hakika, na ambao upeo wa mboni zao sio mbali zaidi kuliko mawingu. Walimwengu hawa wamekuwa vipofu na viziwi kuweza kufahamu ziada iliyopo juu ya upeo wao.

Asiye na macho kwa ajili Yangu hanioni Mimi. Asiye na masikio kwa ajili Yangu hanisikii Mimi. Asiyezirutubisha hisia za harufu, hatahisi harufu ya manukato yamiminikayo kutoka kwenye Uhai, Niliye Ndimi.

Yule mwenye kuzijali tu starehe za ulimwengu huu, haonji riziki zile ambazo maisha ya kila siku humpatia. Anachukua zitokanazo kwa wanyama, kwa maana hata hisia zake za mguso hivyo hivyo hazijarutubishwa wala kupevushwa, na hawezi kugusa uzuri wala ulaini kadri ya mwanga na nuru ya Umungu.

Mwanangu, ninakupenda. Mwanangu, ni mkubwa upendo Nilio nao kwa Wanangu.

Hakuna mwanadamu anayeweza hata kuukadiria Upendo Wangu, maadam hajaweza kuiona kwa macho yake ya kiroho anga katika utukufu wake wa aina nyingi mbalimbali za Uhai Wangu.

Lo tazama, kila kiishicho ndicho kielelezo cha Upendo Wangu. Viumbe vyote hutoa ushuhuda wa Muumba asiyejinafsisha, Niliye Ndimi.

Lo tazama, Mwanangu, kila sogezi la mwili wako, kila pumzi, kila unalohisi na kulinena hutoa ushuhuda wa Nguvu ya Enzi ya milele, Yenye uwezo wote na iliyopo pote.

Hata mwana mwenye kunidhihaki Mimi, mwenye kulikana Jina Langu, mwenye kuvitesa viumbe, lo tazama, Nguvu Yangu imo ndani ya matendo hayo pia, kwani katika vyote imo Nguvu Yangu ndani ya vitu vyote. Ninatoa Nguvu kwa Mwanangu, kwa kila mmoja hivyo hivyo. Huu ndio Upendo usiojinafsisha, ndio Uhai usiojinafsisha.

Lo tazama, kutokana na haya waweza kukadiria jinsi Upendo Wangu ulivyo mkubwa. Mimi silipizi kisasi, Mimi siadhibu kamwe, Mimi hujitolea ndani ya kila mwanadamu, ndani ya kila roho, ndani ya nafsi za Uhai wote.

Kama vile jua lisivyowauliza wanadamu: Je, mnaridhika na jinsi ninavyoangaza? Ama: Mnanikubali ya kwamba ninaangaza?

Lo angalia mwanangu, jua hutoa, na kuutolea mwezi na nyota, ambazo nazo vile vile huitolea dunia na kwa wanadamu. Utaratibu wote wa sayari hutoa, pamoja na dunia. Dunia nayo hutoa. Lo tazama, kutokana na hayo unamtambua katika kiwango kidogo, Yule Mtoaji Mkubwa, Atapakaye pote, yaani Roho wa Upendo.

Mwanangu na mioyo ya wana Wangu yenye kudunda ipasavyo kwa ajili Yangu, hao huzidi kupokea Upendo Wangu kwa maana mioyo yao imenigeukia Kwangu Mimi, kama ulivyo mfano wa ua lenye kujikunjua, na hilo hujikunjua kuelekea mwanga wa jua, ili liweze kujipatia mionzi ya jua kiasi cha kutosha ndani yake.

Lo na uutambue Upendo Wangu usiojinafsisha! Jinsi mwana Wangu anavyojisalimisha Kwangu Mimi, Niliye Uhai usiojinafsisha, na jinsi anavyozidi mwenyewe kutojinafsisha hivyo ndivyo anavyoupokea Uhai huu kutokana na Nguvu isiyojinafsisha, kutoka katika Upendo Wangu, hadi atakapokuwa upendo mwenyewe, atakapokuwa sura Yangu, ndipo basi atakapojiangaza mwenyewe, kuwamulikia wengine wote na viumbe na nafsi za Uhai wote. Mwanangu huu ndio Upendo: Mimi Ndimi, nawe pia unaruhusiwa kuwa.

Na usijinafsishe

Mawazo yenye kujinafsisha, mawazo yanayomzunguka mwanadamu na nafsi yake ni ya kibinadamu. Jinsi mwanadamu anavyojifikiria mwenyewe na anavyofikiria juu ya manufaa yake, ndivyo ufahamu wake unavyopunguka. Yule mwenye kujifikiria mwenyewe tu, bado yuko mbali sana Nami, nisiyejinafsisha.

Mimi Ndimi Uhai usiojinafsisha, ndio Ujazo. Mimi Ndimi Niliye Ndimi ndani ya vyote, pia ndani yako, Mwanangu.

Mimi Ndimi Ujazo, Mimi Ndimi Vyote, na uyaelewe hayo! Ujazo, vyote viishivyo, ndivyo Ndimi, Nami Ndimi Nimo ndani yako. Je, unayaelewa haya? Kama ndivyo mbona unawaogopa watu na vitu vilivyo nje ya nafsi yako iliyo juu? Kutokana na woga unawapatia watu na vitu nguvu za kuuondoa uhuru wako.

Yeyote aliyejinyanyua kuuelekea Uhai usiojinafsisha, huyo husimama juu ya hamu zote za kibinadamu na makusudio mabaya yote, yeye hajinafsishi. Kamwe hajifikiri mwenyewe tena, iwapo hili au lile litamnufaisha. Anatambua ya kwamba anavyo vyote, kwani Ujazo, Mimi, nisiyejinafsisha, ninaishi katika kitovu cha roho yake na katika kila chembe hai ya mwili wake.

Wanangu walio wengi huyahofia ya wakati ujao. Kwa hivyo katika wakati huu, wanayo hayo tu na ambayo wamejigandamisha, au hata kwa upungufu zaidi, kutegemeana na kiwango cha mashaka na woga waliosababisha kwa mipango yao kwa ajili ya wakati ujao. Hivyo, Mwanangu, yule mwenye kuyang'ang'ania mawazo yenye kujinafsisha, huyo anajipunguzisha mwenyewe kwa kujitahidi kujilimbikizia mwenyewe vyote vinavyowezekana ili kukamilisha mipango yake kwa ajili ya kila kitu ambacho kingeweza kutokea wakati ujao.

Na ujinasue kutokana na haya! Utende daima kulingana na Roho Mtakatifu! Wajua wakati ujao wewe utaondoka, kwa hivyo basi hata leo upande mti kwa ajili ya wengine wanaobaki, ili mradi tu uwe na kusudio la ndani ya roho kufanya hivyo. Huko ndiko kuwaza na kutenda kwa roho kusikojinafsisha na kunakoleta uhuru wa Upendo usiojinafsisha.

Yule asiyejifikiria mwenyewe, yule anayetoa tu kutoka katika ujazo wa ndani, yaani mwanga, nguvu, upendo na wemakwa dhati, huyo atakuwa na ujazo kwa wakati wote na hata milele yote.

Milele ndio lengo lako

Wewe ni mwana wa milele. Nawe uyatambue haya!

Hakuna udakizo wa Uhai, kwani vyote ni Uhai. Katika Uhai wote usio na mwisho hakuna kusimama, hata ndani yako katika maisha yako hakuna hivyo.

Wenye kifo tu ni wanadamu na roho zao ambao wamezielekeza hisia na makusudio yao yote katika ulimwengu wa nje, ulimwengu wa kimatirialisti. Siku moja moyo wa roho utajarudi kule ambapo nia zake zipo, yaani kule kwenye ulimwengu wa kimatirialisti, ulimwengu wa starehe na maovu aliouabudu na kudhani kuwa huo ndio nafsi yake ya dhati.

Kwa kiwango cha ufahamu wa mwanadamu ulivyopungukishwa, hivyo hivyo roho itaendelea kuishi kwa njia inayofanana na njia ya awali. Ingawa roho ni mwana wa milele, mwana wa Uhai usio na mwisho, roho hii itaendelea kufungamana na muda na nafasi, na kuyatunza mawazo finyu, na itaendelea kujifikiria ya kwamba ni mwana wa ulimwengu huu na ni mwana wa kimatirialisti.

Na uunyanyue ufahamu wako kwenye anga zote za kiroho kutoka Utaratibu hadi Huruma, nawe uungane na Roho Tapakavu Ambaye Ndiye Vyote katika vyote. Tendo hilo linayaamsha mawazo yako katika kiwango cha milele, ufahamu ambao tu huushuhudia uzuri na usafi usio na mwisho,ambao unaungana pamoja na kila Uhai.

Uzuri wa roho

Uzuri wa roho ni usafi wake. Unajipatia hali hii kutokana na mwenendo bora, ukarimu na mawazo pevu na yasiyojipendelea. Jinsi unavyozidi kutojipendelea, na jinsi mawazo na mwenendo wako vinavyoendelea kuwa bora zaidi, hivyo ndivyo roho yako inavyokuwa na uzuri zaidi.

Ni uzuri na ubora tu utakaoweza kutiririka kutoka kwenye roho iliyo nzuri na safi. Na kutoka kwenye roho iliyojazwa Upendo usio na kujipendelea, ni upendo tu unaoweza kutiririka.

Kutoka kwenye moyo na roho zilizojazwa na Amani Yangu, ni amani tu inayoweza kutiririka, na ni mlingano tu unaoweza kutiririka kutoka kwenye Mlingano, kwani Upendo unaokaa ndani yake umejazwa na Mlingano tu.

Vyote vilivyomo ndani yako ni kielelezo cha nafsi yako, kinachoonyesha tabia na mwenendo wako.

Je, unawezaje kupata uzuri, usafi, upendo na mlingano wa ndani?

Nawe ujitambue ya kwamba, Mimi Niliye Roho wa Uhai, ninakaa ndani yako.

Mimi Ndimi Vyote katika vyote. Mimi Ndimi Niliye Ndimi, Mwenye Uhai. Na uviangalie vyote unavyoviona kwa macho yako ya ndani, kwa macho ya kiroho.

Lo tazama, mara utakapogundua ya kwamba Mimi Ndimi Upendo, Mlingano na Amani katika vyote na katika kila kitu, na ukivikaribisha vyote viishivyo katika upendo, hakuna kipingamizi chochote kitakachotokea dhidi yako.

Uhai ulio safi na bora utaungana na mawazo yako yaliyo safi, bora na yasiyojipendelea, na Uhai huo utatoa zawadi zaidi unavyofikiria. Mwanangu, mara milioni elfu nyingi, Uhai hutiririka kwako kutoka katika nafsi zote za Uhai. Huo ndio Mimi nikupendaye.

Daima wasiliana Nami usiku na mchana, ndipo unapotambua kuwa Mimi Nimo ndani yako, nawe ndani Yangu.

Upendo na utiririke ndani yako, ndipo utakapokuwa kweli mwana uliyebarikiwa kwa ajili ya ulimwengu huu na kwa ajili ya nafsi zote, ndipo utakapoingia kwa uangavu katika Uhai Wangu katika milele.

Milele

Milele, Uhai umefichwa katika nafsi zote.

Ufahamu wako na ufikie kuelekea kwenye sehemu za maumbo asilia, nyota na sayari za mbingu, kwa wanadamu, roho, nafsi na wanyama. Ufahamu wako na utiririke hima, utiririke kuelekea kwenye kimoyo rohoni, ambacho kimo ndani ya nafsi zote za Uhai.

Mfano wa nyuki aingiaye ndani kabisa ya ua lenye kujikunjua, hivyo hivyo ufahamu wako na uzame ndani kabisa ya nafsi zote za Uhai. Usiridhike na kokwa, yaani umatirialisti. Ukiridhika na ganda tu, tena na tena utajifungamanisha na mipaka ya muda na nafasi, maadam unayatazama yaliyo nje kwa macho yako ya kibinadamu.

Nafsi yako ya ndani, hisia zako zilizoamshwa, ufahamu wako na uvitiririshe hata vizame kabisa ndani ya sehemu ya maumbo asilia, ndani ya nyota na sayari za mbingu, na katika nafsi zote za Uhai.

Ndipo kiini cha Uhai, yaani Ndimi, nitakukaribisha. Kutoka hapo utaiona milele, Uhai usio na nafasi wala muda, na utajisikia upo pamoja Nami. Ndipo woga na mashaka vitakuondoka, na kivuli cha kifo kukuondoka, kwa sababu umevipenyeza vitu vya nje.

Kifo

Kifo ni mawazo yaliyofungamana na mipaka. Kifo ni ufahamu wa kiulimwengu uliopunguzishwa.

Yule anayeishi ana kwa ana na mauti, huyo tayari amekwisha kufa kiroho. Anaamini ya kwamba anaishi, lakini haiishi. Maisha yake ni yenye kunyongonyea, yenye mabalaa yasiyoachana na mauti, bali kifo chenyewe kinasababisha mwanzo wake mpya: Kunyong'onyea kwa roho, kuzaliwa mara nyingine tena, kunyong'onyea kwa mwili kisha mabalaa na kifo. Maisha ya namna hii ndiyo bahati yake mbaya ya roho na mwanadamu itakayoendelea hadi mara mwanadamu na roho yake atakapoamka na kufuata njia ya kujifafanua mwenyewe.

Kujifafanua mwenyewe hukuletea uhuru

Na utambue ya kwamba wewe ni mwana Wangu, na ujitegemee dhidi ya nafsi yako mwenyewe na dhidi ya watu wengine, nawe utakuwa huru.

Mwanadamu hataweza kitu akiwa peke yake. Atakachomiliki, atakachokihitaji, ndicho Ndimi.

Lo tazama, Mimi ninajitolea kama sadaka, Mimi Ndimi Vyote katika vyote, Nimo pia ndani ya jirani yako. Mimi ninajitolea kwako wewe pia kupitia watu wakupendao na waliokubali kukutunza katika maisha haya.

Kwa hivyo usimtegemee mtu yeyote kwa fedha wala chochote kile. Chochote upokeacho ukikubali kwa shukrani kunjufu na unione Mimi kama Ndiye Mtoaji.

Usifuje kitu upokeacho. Katika kila kitu ukitumie kwa kiasi, kwani kila kilichotolewa kwako kupitia mtu mwingine wa pili au wa tatu, hicho kinatoka Kwangu.

Mimi ninakuhudumia wewe kupitia kwa jirani yako, kupitia jua, mwezi na nyota, na ninakuhudumia kupitia katika sehemu za maumbo asilia. Chochote kile upokeacho, ukikubali kwa shukrani kunjufu, kwani vyote vilivyo vyema na vyenye upendo hutoka Kwangu.

Mimi ninakutunza wewe usiku na mchana. Mwanangu, ninakulinda, kwani Mimi, Baba yako, ninakupenda. Lo tazama, Mwanangu, yeyote mwenye kuniaminisha Mimi, huyo hupokea. Usikaribishe kila kitu kama mazoea. Na kitu ulicho nacho, ukitumie vema. Ujifafanue mwenyewe tu kama mwana aliyebarikiwa kikamilifu! Walakini, usijilimbikizie zawadi Zangu.

Mimi ninatunza, ninatoa, ninahudumia, ninaponya. Na unitambue Mimi katika vyote na uvikaribishe hivyo vyote kwa shukrani kunjufu, hata kama kwa kufanya hivyo katika muda huo kunakuletea huzuni. Nawe ujue ya kwamba katika mahangaiko hivyo roho nyingi hukomaa.

Na uitimize Sheria Yangu iliyomo katika vyote, ndipo kwa hakika utakapopokea kutoka kwenye ujazo. Yeyote mwenye kuzipigania na kujinyakulia zawadi Zangu, na kuzifikiria kama vitu vyake mwenyewe, akivishikilia akisema: " Mimi, mimi, mimi, mimi tu, vyote kwa ajili yangu!" mwana huyu siku moja atajavipoteza hivyo vyote na atajasimama mbele Yangu, akiwa maskini.

Lo tazama, tendo hili halileti uhuru, ndio ufungwa, kizuizi na jela ya roho. Kulingana na kanuni ya vyanzo na madhara, wale waishio katika kujinafsisha, wanaojifikiria wao wenyewe tu na wanaozitetea zawadi zitokazo Kwangu, na wenye uchu hata wa kupata zawadi zaidi, hao watajakuwa maskini. Wao watajavipoteza vyote, vyote hivyo vitajachukuliwa kutoka kwao kutokana na kanuni ya kupanda na kuvuna.

Kila roho haina budi siku moja kujifafanua yenyewe, utupu na ufichuo wake na nafsi yake ndogo isiyo halali, ambayo haina budi kutolewa sadaka, ili roho ipate uhuru ndani Yangu, Mungu Aliye huru, Mtoaji wa Milele, Ndiye Vyote katika vyote.

Kutoa pasipo kujipendelea

Na usijitetee mweyewe na wala usikitetee kitu chochote ulichopewa tu kuwa nacho na kukitumia.

Yeyote yule ajiteteaye mwenyewe na kuyatetea matoleo Yangu, huyo amejifungamanisha. Yule aliyejifungamanisha hawezi kujipatia mwenyewe uhuru, ila pasipo kujitolea mwenyewe Kwangu Mimi, Mwenye Milele.

Mwanangu, na ujitolee mwenyewe kupitia katika Upendo Wangu. Lo tazama, Upendo una nguvu kushinda yote katika anga, huu Upendo hujitolea sadaka daima.

Kila ulitendalo linapaswa kupenyezwa na Upendo usiojinafsisha. Hilo litawezekana tu, iwapo hutaangalia nje ya mwili, bali katika kimoyo cha kila roho.

Angalia ndani ukivipenyeza vitu vya nje na uungamane pamoja na kimoyo rohoni, pamoja Nami, Niliye Uungu. Ndipo utakapokutana na usafi tu, ndipo utakapoona upendo tu. Kutoka hapo wewe utaweza pia kutoa upendo tu, kwa sababu usafi na upendo vinawasiliana ndani ya moyo wako usiojipendelea, ndipo utakapoishi pasipo kujinafsisha kadri ya sheria.

Na usijinafsishe!


[ Book Index ] [ Uzima Liwaza Homepage ] [ Mail ]
[
Order Free Info ]


Universelles Leben e.V., P.O.Box 5643, D-97006 Würzburg
Germany Phone: (+49) 931-3903-0 , Fax: (+49) 931-3903-233
email: info@universelles-leben.org
[an error occurred while processing this directive]